HELIKOPTA
ya Chadema maarufu kama Chopa, juzi ilipotea angani na kusababisha viongozi wa
chama hicho kushindwa kufanya mkutano katika Kijiji cha Mpwayungu wilayani
Chamwino, kama ilivyokuwa imepangwa kwenye ratiba.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyokuwa imepangwa, viongozi wa kitaifa ambao ni Mwanasheria
Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (BAVICHA),
walikuwa wafanye mkutano katika kijiji hicho saa 4 asubuhi.
Akizungumza
na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Steven Massawe alikiri
kupotea kwa helikopta hiyo na kukanusha kwamba hakuna njama zozote zilizofanywa
na CCM kutokana na kupotea kwa helikopta hiyo.
Kijiji
cha Mpwayungu kipo katika Kata ya Mpwayungu, ambayo nafasi ya udiwani ipo wazi
na vyama vya Chadema na CCM vyote vimesimamisha wagombea.
“Sababu
kubwa ya kupotea kwa helikopta ni tatizo la mawasiliano kama mnavyojua Kijiji
cha Mpwayungu hakina mawasiliano. Helikopta ilikuwa ifike katika Kijiji cha
Mpwayungu saa nne asubuhi, lakini Kapteni alipotea na kusababisha kukaa angani
kwa saa moja na dakika arobaini na akatua Kijiji cha Chipogolo.
“Alipofika
Chipogolo akaambiwa sio kijiji hicho chenye mkutano na akatakiwa kurudi nyuma
kwa upande wa magharibi kwa kilometa 40, hata hivyo hakufanikiwa ikabidi arudi
mjini kujaza mafuta,” alisema Massawe.
Alisema
baada ya kujaza mafuta, viongozi hao hawakwenda tena kufanya mkutano Mpwayungu
badala yake wakaenda Mpwapwa ambapo kulikuwa na mkutano mwingine saa 7 mchana
kwa mujibu wa ratiba.
“Leo
(jana) hii viongozi hao kwa kutumia helikopta wamekwenda tena Mpwayungu na
kufanikiwa kufanya mkutano majira ya saa nne asubuni na baada ya hapo waliekea
Kijiji cha Segala Wilaya ya Chamwino, baadaye wataenda Kiteto na Moshi,”
alisema.
Alisema
sio kweli kwamba CCM walifanya njama helikopta ya Chadema ipotee ili isifanye
mkutano katika kijiji hicho na kwamba Chadema na CCM vyote vilishafanya
uzinduzi wa kapteni katika kata hiyo.
“Chadema
ilifanya uzinduzi wake wa kampeni katika Kata ya Mwayungu, Januari 26 mwaka huu
na CCM walifanya uzinduzi wao Januari 20,” alisema Massawe.
Naye
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa,
amesema iwapo Serikali ya CCM haitaweka mazingira ya haki kwa makundi
mbalimbali ndani ya jamii kwa ajili ya amani ya kudumu, migogoro ya ardhi
italitumbukiza taifa katika sintofahamu na hatari kubwa nchini.
Dk.
Slaa aliyasema hayo kwenye mikutano ya M4C Pamoja Daima, jana alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Iselamagazi, Kishapu, Mhunze, Itilima, Lugulu
na Bariadi.
Alisema
ni haki kwa wananchi kuwa na matumaini, kwani ndiyo misingi wa amani ya kweli
ambayo haihitaji kuhubiriwa jukwaani.
Chama cha mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kinashangazwa na kitendo cha chama cha
demokrasia na maendeleo (Chadema)kutumia Helikpota kwenye chaguzi zake huku
kikidai kuwa ni mkombozi wa wananchi jambo ambalo ni kujitafutia sifa na
umaarufu pekee kwa wananchi.
Hayo
yameelezwa na Naibu Katibu mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Mwigulu
Nchemba wakati akifungua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya Sombetini .
Mwigulu alisema kuwa CCM inashangaa sana Chadema kutumia Helikpota kwenye
chaguzi nyingi hapa nchini jambo ambalo wanaonesha wazi kuwa wanatumia gharama
kubwa kwa ajili ya kuongeza sifa kwani gharama ambazo zinatumika hadi
kumalizika kwa kampeni ni zaidi ya Milioni 200.
Pia aliwataka wananchi kuhakikisha kuwa kamwe hawatumiki kwenye siasa za sifa na ushahbiki kwani siasa hizo wakati mwingine zinasababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia ya kufa ovyo: “wananchi mnapswa kujua na kutambua kuwa siasa za sasa zimebadilika sana msikubali kuwa mashabiki wa siasa bali mnatakiwa kuangalia zaidi sera za vyama na mahitaji yenu msije mkachagua kiongozi kwa ushabiki itawagharimu sana kwenye utendaji”aliongeza Mwigulu
Awali
Mgombea Udiwani katika kata hiyo ya Sombetini kwa tiketi ya CCM Bw David Mollel
alisema kuwa ana mikakati mingi sana ya kuhakikisha kuwa anasaidia kata hiyo
endapo atapata ridhaa ya kuongoza rasmi kama diwani .David alisema kuwa
changamoto ambazo atahakikisha kuwa anazitatua ni pamoja na urekebishaji wa
barabara, uboreshaji wa masoko,kna uimarishaji wa vikundi vya wanawake na jamii
kwa ujumla
No comments:
Post a Comment