EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, January 31, 2014

VITABU CHENJI YA RADA VYAKAGULIWA NA PAC DARE ES SALAAM





Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014, akikagua vitabu vya ziada.

Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa kutokana na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake ilikuta vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi.

Wanafunzi wakisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, kwenye shule ya msingi Bunge katikati ya jiji la Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014.Picha na K-Vis Blog.


No comments:

Post a Comment