EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, December 13, 2013

KIFAA KINGINE CHA SIMBA SC KUTOKA KENYE HIKI HAPA

Klabu wekundu wa msimbazi  SIMBA SC, imefanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, beki wa kati wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Donald Mosoti Omwanwa, ambaye ni pendekezo la kocha wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic pamoja na kipa Ivo Mapunda.

 
Katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala Amesafiri hadi Nairobi kwaajili ya  beki huyo na kumsainisha Mkataba wa miaka miwili kuichezea simba

Akizungumza  beki huyo mrefu alisema kwamba anashukuru kujiunga na Simba SC, kwani ni klabu kubwa na ya kihistoria Afrika Mashariki.

“Nimefurahi kusaini Simba SC, hii ni klabu kubwa na ya kihistoria ukanda huu wa Afrika Mashariki, nataka kufuata nyayo za Wakenya wengine waliochezea klabu hii kwa mafanikio kama Mark Sirengo, Hillary Echesa na Mike Barasa,”alisema.


Mchezaji huyo anayetarajiwa kuondoka leo kwenda Dar es Salaam kujiunga na wenzake, alisema kwamba amefurahi pia kwenda kufanya kazi tena chini ya kocha Logarusic, ambaye alikuwa mwalimu wake Gor Mahia.


 “Mimi binafsi kama mchezaji ni faraja kwenda kufanya tena kazi na Loga, ni kocha mzuri na aliifanya Gor iwe na heshima hapa (Kenya) na hata Simba SC wajue wamepata kocha mzuri,”alisema.
 
Donald Mosoti Omanwa alizaliwa Julai 14, mwaka 1981 kijiji cha Kisii, Nyanza nchini na Kenya na alipata elimu yake ya Msingi na sekondari huko huko Kisii.

  Kisoka, baada ya mpira wa shule, beki huyo alianzia klabu ya World Hope ya Nairobi mwaka 2005 kabla ya kuhamia Nairobi City Stars mwaka 2008 ambako alicheza hadi mwaka 2011 alipojiunga na Gor Mahia.

Omwanwa alisema Mkataba wake wa sasa na Gor Mahia unamalizika Februari 31, mwakani lakini ameruhusiwa kusaini Simba SC kwa kuwa Ligi ya Kenya inaanza Machi mwakani

Donald Mosoti Omanwa  aliye vaa blue  uzi wa Gormahia 

 


No comments:

Post a Comment