NA MSHAM, NGOJWIKE
UONGOZI wa vyama vya Soka
mikoani umeshauriwa kuanzisha Ligi ya wanawake kwa ajili ya kuendeleza na
kukuza mchezo huo ambao uneonekana kuwa ni wa wanaume pekee.
Ombi hilo limetolewa na Kocha
Mkuu wa Timu ya Taifa ya wasichana chini ya miaka 17 ‘Tanzanite’ ambayo
inashiriki kwenye michuano ya kusaka tiketi ya mucheza fainali za kombe la
Dunia zitakazochezwa mwakani nchini Canada.
Akizungumza na BINGWA juzi
kocha huyo alisema kuwa ni muhimu kuhamasisha soka la wanawake hasa kwa kuanzia
mikoani kwa kuanzisha Ligi ndogo ndogo ambazo baadaye kupata timu zinaoeleweka
na kuzisajili.
“Hatuwezi kupata jibu la
kwanini soka la wanawake halipewi kipaumbele hadi pale tutakapoamua kutafuta
njia za kuliinua na kuliendekeza kuanzia mikoani” alisema.
Kaijage alisema kwamba mchezo
huo umeonekana kuwa kama ni wa wanaume pekee ambapo inawafanya hadi na
wasichana wenyewe wanaoshiriki mchezo huyo kutaka kujifananisha na wanaume.
Tanzanite kwa sasa inaendelea
kujiandaa na mechi yao ya marudiana dhidi ya timu ya Taifa ya Msumbiji
itakayochezwa hivi karibuni nchini humo, baada ya kushinda katika mechi yao ya
kwanza iliyochezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment