MENEJA wa klabu ya
Manchester City, Manuel Pellegrini amesema golikipa namba moja wa timu
hiyo Joe Hart anahitaji muda wa kupumzika baada ya kumuacha katika
mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Norwich City. Hali
hiyo imekuja kufuatia Hart mwenye umri wa miaka 26 kufanya makosa ya
kizembe katika mechi za karibuni alizocheza hivyo kuigharimu timu hiyo. Akihojiwa
Pellegrini na mtandao wa timu hiyo amesema jukumu lake ni kuangalia
kila wiki mchezaji gani ni bora kwa ajili ya kucheza. Kocha
aliendelea kudai kuwa Hart anahitaji mapumziko na yataweza kumsadia
kwasababu amecheza katika kila mechi kwa kipindi cha miaka miwili
iliyopita na kila mchezaji hupitia kipindi kibaya. Amesema
anachotakiwa kufanya Hart hivi sasa ni kujituma kwa bidii ili aweze
kurejea katika kiwango chake na atakuwa pamoja nae katika kipindi chote.
No comments:
Post a Comment