NA ,MSHAM NGIJWIKE
MSHAMBULIAJI wa Mbeya
City,Paul Nonga amesema kuwa wale wanaodhani kasi ya timu yao ni nguvu ya soda
watafunga midomo yao ligi itakapomalizika.
Mbeya City ambayo imepanda
daraja msimu huu imekuwa mwiba mchungu kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ambapo
mpaka sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.
Akizungumza na BINGWA jana
kutoka jijini Mbeya,Nonga alisema kuwa baadhi ya watu wanafikiri timu yao
itapunguza kasi mbele ya safari kwani ndio kwanza wamepanda daraja lakini
akasisitiza kwamba lengo lao ni kuchukua ubingwa.
“Watu wengi wanadhani kwamba
kasi tuliyonayo itakuja kupungua mbele ya safari lakini mimi nawaambia
tumedhamiria kuchukua ubingwa msimu huu licha ya kwamba ndio kwanza tumepanda
daraja,” alisema.
Nonga ambaye alisajiliwa na
timu hiyo akitokea kwa JKT Oljoro ndiye anayeongoza katika timu hiyo kwa
kufunga mabao ambapo ameshafunga mabao manne mpaka sasa.
Mbali na kudai timu yake
itaibuka bingwa msimu huu,pia Nonga amesema kwamba dhamira yake ni kuibuka
mfungaji bora na kuwafunika Amis Tambwe wa Simba anayeongoza pamoja na Hamis
Kiiza wa Yanga.
No comments:
Post a Comment