NA EZEKIEL TENDWA
CHAMA cha ngumi Mkoani Arusha
(AABA) kimeandaa mashindano yajulikanayo kama Uhuru Cup yatakayoshirikisha timu
za ukanda wa Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9 hadi 12 jijini
Arusha.
Akizungumza na BINGWA jana
kutoka jijini Arusha,Katibu mkuu wa AABA,Mohamed Abubakar alisema kuwa
maandalizi yanakwenda vizuri huku wakipata sapoti kubwa kutoka kwa wadau
mbalimbali.
“Tutakuwa na mashindano
ambayo tumeyapachika jina la Uhuru Cup yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 hadi
12 mwaka huu hapa Arusha na jambo la kushukuru tunapata sapoti kubwa kutoka kwa
wadau mbalimbali,” alisema.
Alisema baadhi ya timu ambazo
zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo ni timu kutoka Kampala nchini
Uganda,Nairobi pamoja na Mombasa kutoka nchini Kenya,Mwanza,Dar es Salaam
pamoja na wenyeji Arusha.
Katika hatua nyingine alisema
kwamba wanatarajia mabondia wao wataonyesha mchezo mzuri kama walivyofanya
katika mashindano ya majiji yaliyofanyika Nairobi Kenya mwanzoni mwa mwezi
uliopita.
“Mwanzoni mwa mwezi uliopita
katika michuano ya majiji yaliyofanyika Nairobi nchini Kenya tulifanikiwa
kuibuka na medali tatu sasa kipindi hiki tupo nyumbani tutafanya vizuri zaidi,”
alisema.
No comments:
Post a Comment