EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, October 31, 2013

UNESCO:VIJANA MILL 2.6 TANZANIA WANAISHI NA VVU UKIMWI



IMEELEZWA kuwa Vijana milioni 2.6 wenye umri wa miaka kati 15 na 24 hapa nchini, wanaishi na virusi vya Ukimwi. 


Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Abdoul Coulibaly,  ametoa takwimu hizo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa taarifa ya elimu ya jinsia na afya ya uzazi kwa vijana katika nchi 21 za Mashariki  na Kusini  mwa Afrika.
Amesema kuwa karibu vijana 50 kutoka katika nchi hizo huambukizwa virusi vya Ukimwi kila saa moja, huku idadi ya wasichana wakiongoza kwa maambukizi hayo.

Coulibaly amesema idadi hiyo ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana kwa Tanzania, inachangiwa  na kutokuwapo kwa elimu ya kutosha ya jinsia  pamoja na VVU na Ukimwi, afya ya uzazi na ukuaji wa binadamu, jambo ambalo husababisha kujiingiza  kwenye mapenzi katika umri mdogo na kusababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni.
Mwakilishi huyo wa UNESCO ameiomba serikali kuweka mikakati madhubuti ya kutoa elimu ya afya na jinsia kwa vijana, kwa ajili ya kusaidia kupunguza idadi ya maambukizi kwao, pamoja na mimba za utotoni zinazosababishwa na ukosefu wa elimu hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi, kitengo cha masuala mtambuka kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Laetitia Sayi, amesema changamoto ya maambukizi ya VVU kwa vijana ni kubwa, na kwamba serikali kwa upande wake inafanya jitihada mbalimbali za kutatua tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment