EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, October 31, 2013

MBOWE:SI RUHUSA NYUMBA ZA IBADA KUWA MAJUKWAA YA SIASA


Mbowe-mwenyekiti chadema

RAI imetolewa kwa viongozi wa dini kukemea watu wanaogeuza nyumba za ibada, kama njia ya kutaka kufanikisha malengo yao ya kisiasa kwa kutoa michango ya fedha wanazozipata kwa njia ya ufisadi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ametoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Sono uliopo katika kijiji cha Masama-Sono, wilayani Hai, mkoa wa Kilimanjaro.
 


Amewataka viongozi wa dini zote nchini kukemea suala hilo na wawe makini na watu wa namna hiyo, badala ya kuangalia kiwango cha ukubwa wa fedha wanazotoa bali uhalali na usafi wa kile wanachochangia.
Naye Askofu Mkuu mstaafu wa KKKT, Erasto Kweka, amemshukuru mbunge huyo na akimtaka aendelee na moyo huo kwa kuitikia wito wa kujumuika na waumini wa usharika huo na kuwatia nguvu katika ujenzi wa kanisa lao. Takriban Sh. milioni 16 zilichangwa kwa fedha taslimu na ahadi, katika harambee hiyo, ambapo waumini wa usharika huo walichangia jumla ya Sh. 7,956,800 huku mbunge huyo akichangia Shilingi milioni nane.


No comments:

Post a Comment