Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kesho mchana anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kutokana na ratiba hiyo Serikali imewaelekeza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge.
![]() |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania |
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amethibitisha jana katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kuwapo kwa ratiba ya Rais Kikwete kesho Alhamisi kulihutubia Bunge. Rais Kikwete atalihutubia Bunge wakati likisubiri kujadili mapendekezo ya marekebisho katika Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2013, ambayo ilipitishwa katika mkutano uliopita.

No comments:
Post a Comment