TOTTENHAM WALICHEMKA KUNISAJILI - PATO.
MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Corinthians Alexandre Pato amethibitisha kuwa Tottenham
Hotspurs walishindwa ofa yao ya kutaka kumsajili katika kipindi cha
usajili majira ya kiangazi. Akihojiwa
kuhisiana na hilo Pato amesema Tottenham waliwasiliana na Corinthians
kuhusu uhamisho wake lakini yeye na wakala wake waliamua kuwa anahitaji
kubakia hapo. Nyota
huyo wa kimataifa wa Brazil aliibukia barani Ulaya wakati akiwa na umri
wa miaka 17 mwaka 2007 wakati alipoifungia bao timu yake ya AC Milan
katika mchezo wa Serie A dhidi ya Napoli. Pato
alifanya vyema katika msimu wa 2010-2011 wakati alipoifungia Milan
mabao 14 lakini aliporomoka ghafla baada ya kuanza kuandamwa na majeruhi
ya mara kwa mara yaliyopelekea kuamua kurejea nchini kwao Brazil.
No comments:
Post a Comment