SHIRIKISHO la Soka
Duniani-FIFA limeruhusu timu ya taifa ya Misri kucheza mchezo wake wa
mkondo wa pili wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ghana
katika jijini la Cairo pamoja na hofu ya hali ya usalama. Chama
cha Soka cha Ghana-GFA kilituma maombi FIFA ya kutaka kutafutwa uwanja
mwingine ambao utakuwa salama kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika
Novemba 19 mwaka huu. Hata hivyo, FIFA ilithibitisha jana kuruhusu mchezo huo uchezwe jijini Cairo baada ya wakaguzi kuhakikisha hali ya usalama. Mshindi katika mchezo huo wa mtoano atafuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment