EBENEZA MARCH 9 2014
SWACO
royal
tt
NIMO
mvuto
Wednesday, October 16, 2013
RWANDA YAPOTOSHA TAARIFA ZA USALAMA NA HAKI
Bodi ya utawala ya Rwanda imeilaani ripoti ya mwaka 2013, iliyotolewa na shirika la Mo Ibrahim kuhusu mambo ya utawala katika nchi za Afrika, kwa kupotosha takwimu kuhusu usalama, ushiriki na haki nchini Rwanda.
Taarifa hiyo iliyotolewa siku ya jumatatu huko London, katika kipengele
cha usalama wa taifa imeiweka Rwanda katika nafasi ya 49 miongoni mwa nchi 52 na kuipa asilimia 50.4. Katika kipengele cha ushiriki imewekwa ya 46 na kupewa asilimia 16 na haki za binadamu nafasi ya 45 ikipewa asilimia 27.5.Akizungumza na shirika la habari la China Xinhua, Afisa mkuu mtendaji wa bodi hiyo Anastase Shyaka, amesema shirika hilo limetoa takwimu zisizo sahihi kuhusu usalama, ushiriki na haki ambazo haziendani kabisa na hali halisi ya Rwanda. Amesisitiza kuwa Rwanda ilipata maendeleo katika maeneo hayo matatu. Hata hivyo ripoti hiyo ya mwaka imeiweka Rwanda katika nafasi ya 5 kati ya nchi zilizofanya vizuri zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment