![]() |
| Rais wa malawi Joyce Banda |
Rais Joyce Banda wa Malawi jana alitangaza baraza jipya la mawaziri baada ya kuvunja baraza la zamani lililokumbwa na tuhuma za kufanya udanganyifu na ufisadi. Katika baraza jipya, waziri wa fedha Bw Ken Lipenga ameachwa na nafasi yake imechukuliwa na Bw Maxwell Mkwezalamba. Pia amemteua Bw Fahad Assan kuwa waziri wa sheria na katiba badala ya Bw Ralph Kasambara.Kuanzia mwezi Septemba maofisa kadhaa wa serikali katika hazina ya taifa, mkaguzi wa serikali, ofisi ya rais na baraza la mawaziri wamekuwa wakikamatwa kutokana na kuhusika na ufisadi wa mamilioni ya dola za kimarekani.

No comments:
Post a Comment