EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 16, 2013

VITA NCHINI KONGO NA M23 YAANZA UPYA TENA KWA KASI


kikosi cha waasi wa M23

Mapigano kati ya waasi wa harakati ya Machi 23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameanza tena hii leo.Ripoti zinaarifu kuwa hadi jioni ya leo mapigano yalikuwa yakiendelea huko Kibumba umbali wa kilomita 15 kutoka mji wa Goma kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23. Msemaji wa jeshi la Kongo amethibitisha kutokea mapigano hayo na kutangaza kuwa jeshi hilo limejizuia kutekeleza mashambulizi lakini akasema kuwa waasi wa Machi 23 watakabiliwa na mashambulizi ya jeshi la Kongo iwapo wataendeleza uchokozi.
 
kikosi cha waasi wa M23
Waasi wa harakati ya Machi 23 pia wamelituhumu jeshi la Kongo na kusema kuwa jeshi hilo ndilo lililoanzisha mashambulizi hayo ya leo. Ni muda sasa maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanashuhudia harakati za wanamgambo wenye silaha hususan wale wenye uhusiano na waasi wa M23.

No comments:

Post a Comment