EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 12, 2013

RAISI JAKAYA KIKWETE NA NDOA ZA UMRI MDOGO TANZANIA



Serikali imesema kuwa inaangalia uwezekano wa kubadili sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 15, na badala yake iruhusu umri wa kuolewa uanzie miaka kumi na nane.
Hayo yameelezwa jana jijini Dar es salaam na waziri wa katiba na sheria Mathias Chikawe, wakati akizingumza katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusiana na ndoa za utotoni, ambapo jana ilikuwa ni siku ya mtoto wa kike duniani.
katiba ya Tanzania

Waziri Chikawe amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya sasa mtoto wa miaka 15 anaruhusiwa kuolewa kwa idhini ya wazazi wake, jambo ambalo amewataka wadau wote kushirikiana ili kuhakikisha sheria itambue umri wa ndoa uwe ni miaka 18 na si vinginevyo.
Amesema kuwa ndoa za utotoni kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kik,e kutokana na wengi wao kuachishwa shule na kuozeshwa.Hata hivyo Waziri Chikawe ameeleza kuwa suala la kubadili sheria hiyo linatarajiwa kuchukua zaidi ya miaka mitatu, ili kukomesha kabisa ndoa za utotoni.

No comments:

Post a Comment