EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 12, 2013

RAISI KIKWETE AISHAURI MBEYA KULIMA KILIMO CHA MBOGAMBOGA



Idara ya Kilimo mkoani Mbeya ikishirikiana na Chuo cha Kilimo cha Uyole, imeanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuutaka mkoa huo utenge maeneo kwa ajili ya kilimo cha mboga na matunda, ili kuinua mapato ya mkoa huo. 
Raisi Jakaya Kikwete akihutubia
Afisa mkuu wa kilimo mkoani humo Enock Nyasebwa, amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo unahusisha kuanza kutafuta maeneo maalumu ya skimu za bustani kwa ajili ya kilimo hicho.Afisa huyo amesema mkakati mwingine utakaotumika ni kuwaunganisha wakulima katika chama kimoja cha ushirika, kufanya tathimini ya uzalishaji wa mboga na matunda, na kuwapo kwa soko la uhakika.
Eneo la Mbeya ni moja wapo ya maeneo ambayo yametengwa na serikali, ili kutumika kuendeleza chakula cha mboga na matunda katika harakati za kuinua uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment