![]() |
| waumini wa kiislam wakiwa katika ibada Makka |
Maelfu ya mahujaji wa kiislamu wamekusanyika katika
mji mtukufu wa Makka nchini Saudi Arabia katika ibada ya kila mwaka ya Hajj,
huku maafisa wa nchi hiyo wakionya dhidi ya kuingizwa siasa ndani ya mkusanyiko
huo mkubwa duniani.
Imam wa msikiti mkuu wa Makka Sheikh Saleh bin
Mohammed al-Taleb, amewataka waislamu duniani kote kuungana pamoja na kumaliza
mizozo.
Hijja ni nguzo ya mwisho katika nguzo tano za
Uislamu inayomhimiza kila mwenye uwezo kufanya Hijja,
![]() |
| Msikiti mtukufu wa Mkka |
kufanya hivyo angalau
mara moja maishani mwake.Maafisa nchini humo wanasema tayari mahujaji
takriban milioni 1.4 wameshawasili kwa ibada hiyo, ingawa idadi hiyo ni ndogo
ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo takriban mahujaji milioni 3.2
walihudhuria.
Inasemekana Matatizo ya kupumua kutokana hali mbaya
ya joto ni moja wapo ya sababu za kupungua kwa idadi ya mahujaji
mwaka huu.


No comments:
Post a Comment