EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 9, 2013

MZOZO WA BAJETI UNAVYOMCHANGANYA RAIS OBAMA



                                            NEW YORK
Rais Barack Obama  wa  Marekani amewaalika  wabunge wa  baraza  la  wawakilishi  kutoka  chama  chake  cha Democratic,  kukutana  nae  leo ili  kujadili  mzozo  wa bajeti  na hali  inayokaribia  ya  muda  wa  mwisho  wa kulipa  madeni.

Afisa  wa  Ikulu  ya  Marekani  amesema kuwa  huu  utakuwa  mwanzo  wa  mazungumzo  kadhaa anayotarajia  kuyafanya  na  wabunge  wa  vyama  vyote.Afisa  huyo  amesema  kuwa  makundi  mengine  ya wabunge , ikiwa  ni  pamoja  na  wale  wa  Republican kutoka  mabaraza  yote  ya  bunge  la  Marekani, yaani Congress, wataalikwa  katika  siku  zinazokuja.
Ikiwa  hakuonekani kupatikana suluhisho  hivi  karibuni katika  mzozo  huo  wa  bajeti  ulioanza  kuyumbisha masoko  ya  hisa , mkutano  huo unaashiria  mwanzo  wa juhudi  za  kuepusha  hatua  ya  kushindwa  kulipa  madeni, ambapo  imebakia  wiki  moja   kabla  ya  muda  wa mwisho  kumalizika.Obama  ameonya   kuwa kutatokea  mparaganyiko  na matatizo  makubwa  ya  kiuchumi iwapo  taifa  hilo litaruhusiwa   kufikia  hatua  ya  kushindwa  kulipa  madeni yake.

No comments:

Post a Comment