EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 9, 2013

MOHAMMED MURSI KUFIKISHWA MAHAKAMANI NOVEMBER 4



                                            
waandamanaji misri wakiwa wamebeba picha ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Muhamad Muls
CAIRO

Rais Mohammed Mursi aliyeondolewa  madarakani  nchini Misri, atafikishwa  mahakamani  Novemba  4 kwa  madai  ya kuchochea mauaji  ya  wapinzani  wake  wakati  akiwa madarakani.
Mahakama  ya  Misri  imesema  leo  kuwa Mursi pamoja  na  wanachama  wengine  14  wa  chama chake  cha  Udugu  wa  Kiislamu,  watafikishwa mahakamani , ikiwa  ni  pamoja  na  wasaidizi  wa  ngazi  ya juu  na  wanachama  waaandamizi  wa  kundi  hilo.
misri wakati wa machafuko

Mursi  aliondolewa  madarakani  katika  mapinduzi Julai  3  mwaka  huu,  na amekuwa  akishikiliwa  mahali  pasipojulikana na hajaonekana  tangu  wakati  huo, licha  ya  kuwa amezungumza na  familia  yake  mara  mbili,  na alitembelewa  na  mkuu  wa  sera  za  mambo  ya  kigeni wa  Umoja  wa  ulaya  Catherine Ashton , pamoja  na ujumbe  wa  Umoja  wa  Afrika.
Mahakama  hiyo  ya  rufaa ya  mjini  Cairo  imemtaja  jaji Ahmed Sabry Youseff kuendesha  kesi  hiyo.

No comments:

Post a Comment