PRETORIA.
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bibi
Maite Nkoana Mashabane, amesema kuwa Umoja wa Afrika utaamua kama nchi za
Afrika zitabaki katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai au la. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Pretoria kuhusu mkutano usio wa kawaida wa Umoja wa Afrika, utakaofanyika alhamisi na Ijumaa, bibi Mashabane amesema Afrika Kusini itaunga mkono uamuzi wowote utakaochukuliwa na Umoja wa Afrika.
Mkutano huo utajadili ushiriki wa nchi za Afrika katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai.
Nchi kadhaa za Afrika zimetishia kujitoa katika mahakama hiyo na kuishutumu kwa kuwalenga waafrika, ikiwa ni pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, ambao kesi yao inaendelea katika mahakama ya hiyo, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu zaidi ya 1000 katika vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

No comments:
Post a Comment