EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 29, 2013

Marekani yakiri haja ya vikwazo kwa kazi za NSA

Rais Barack Obama wa Marekani anataka kazi za ukusanyaji wa taarifa za kijasusi zifuatiliwe kufuatia kashfa ya hivi karibuni ya unasaji wa mawasiliano uliofanywa na Shirika la Usalama la nchi hiyo, NSA. 
Rais Barack Obama wa Marekani


Obama alibainisha hapo jana kwamba shughuli za shirika hilo zitaangaliwa upya, ili kuhakikisha kwamba halifanyi tu, kila kile ambacho lina uwezo nalo kiufundi. 

Kauli ya Rais Obama ilitanguliwa na ya msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jay Carney, aliyewaambia waandishi wa habari kwamba licha ya matumizi ya teknolojia mpya kulinda maslahi ya kiusalama ya nchi hiyo, hayapaswi kukiuka dhima yake. 

Kauli hiyo ya hapo jana inachukuliwa kama jibu la jumla hadi hivi sasa kuwahi kutolewa na serikali ya Marekani dhidi ya hasira zilizoenea kutokana na programu ya ujasusi ya Shirika la NSA.

No comments:

Post a Comment