Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameushukuru Umoja wa Afrika, kwa uungaji mkono mkubwa waliouonesha kwa Kenya, kuhusu kesi inayowakabili viongozi wa nchi hiyo kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai.
![]() |
| Rais wa keny uhuru kenyata |
Katika taarifa aliyoitoa jijini Nairobi baada ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa umoja wa mataifa mjini Addis Ababa, uliokuwa unapitia uhusiano kati ya Umoja wa Afrika, na Mahakama ya kimataifa ya makosa ya Jinai ICC.
![]() |
| kenyata akihutubia |
Rais Kenyatta amesema azimio lililopitishwa na viongozi wa nchi za Afrika ni ishara ya wazi kuwa, bara la Afrika liko tayari kujiamulia mustakbali wake.Rais Kenyatta amesema Umoja wa Afrika na nchi mbalimbali za Afrika, zina haki ya kulinda uhuru wao na kujiamulia mambo yao. Amesema kuwa nchi za Afrika zilijiunga na mahakama hiyo kwa hiari na kwa nia njema, lakini sasa inaonekana kuwa nchi za Afrika zimekuwa windo la nchi za magharibi ambazo zinaendesha mahakama hiyo.


No comments:
Post a Comment