EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, October 14, 2013

BENKI YA DUNIA YAIKWAMUA TANZANIA KWA PESA NONO



                                            GENEVA.
Benki ya Dunia imetoa mkopo wa dola milioni 340 kwa nchi tatu za Kiafrika za Tanzania, Burundi na Rwanda, zitakazotumika kwa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme katika eneo la Rusumo.
Taarifa zinasema kuwa, bwawa hilo la kuzalisha umeme litakamilika mwaka 2020, ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 80 za umeme. 


Mawaziri wa Fedha wa nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda wametia saini makubaliano ya utekelezwaji wa mradi huo, ambao unadhaminiwa na Benki ya Dunia.Mradi huo utasaidia kuongeza nguvu za umeme katika nchi hizo tatu, ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
 
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, ujenzi wa bwawa hilo la umeme kwa kiasi kikubwa utaziba ufa ambao ulianza kujitokeza kwenye uhusiano wa Tanzania na Rwanda katika miezi ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment