Ofisa wa Palestina amesema hakuna taarifa
mpya zilizotolewa kuhusu chanzo cha kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa mamlaka ya
utawala wa Palestina Yasser Arafat.
Tawfi Al Tirawi, mkuu wa kamati iliyokuwa inachunguza
chanzo cha kifo cha Arafat amesema habari zilizotolewa na jarida moja la Uingereza
zinazosema kifo cha Arafat kilitokana na sumu, si habari mpya kwani habari hizo
zinatokana na ripoti iliyoandaliwa na televisheni ya Al Jazeera.
Amesema hadi sasa wanaendelea kusubiri
taarifa rasmi kutoka kwa wachunguzi.Kutokana na ripoti ya televisheni ya Al
Jazeera iliyosema kifo cha Arafat kilitokana na sumu aina ya polonium 210, na
nguo zake ziligunduliwa kuwa na sumu hiyo.Kutokana na habari hizo mwezi Novemba mwaka
jana wataalamu wa Ufaransa, Uswisi na Urusi walifukua mwili wa Arafat na
kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

No comments:
Post a Comment