
Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume
wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa
mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza
kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi
Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye
wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo
ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.
Bishosti huyo alisema kuwa
tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado
wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi
kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani...
BBA: MSHIRIKI WA TANZANIA ( NANDO) HUENDA AKASHITAKIWA KWA KOSA LA KUMDHALILISHA MSHIRIKI WA KIKE TOKA GHANA

Mshiriki wa pekee katika Jumba la BBA
The Chase , Selly kutoka nchini Ghana, amesema ya kwamba yupo mbioni
kumfungulia mashtaka mshiriki kutoka nchini Tanzania Nando kwa kitendo
cha kumdhalilisha na kumsingizia amemuambukiza Ugonjwa wa Zinaa.Baada
ya kutolewa katika jumba hilo wiki iliyopita, Selly ameshauriwa na mama
yake na tayari wamewasiliana na Waandaji wa Shindano hilo. " Nimepima
sijakutwa na maambukizi ya aina yoyote ya Magonjwa ya Zinaa wala sina
historia hiyo" Alisema Selly." Mimi na Nando hatukufanya Mapenzi
zaidi ya kucheza tu Kitandani, nashangaa hata kwa kiasi gani mambo
yamekuwa hivi" Aliongeza Mrembo huy...
CHRISTOPHER GEORGE YOHANA NI ASKARI WA TANZANIA ALIYETEKWA NA WAASI WA M23

Waasi wa M23 wa DR Congo, wanadai kuwa wamemkamata askari wa Tanzania
anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa
Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka
1994.
Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Kwa mujibu wa chimpreports.com,
M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47
yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook
ikiambatana na picha hiyo:
“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka
Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko
Rutshuru....
MUME AZIMIA BAADA YA MKE WAKE KUNASWA AKIJIUZA

Mume na mke wakiongea
Seleman Yasin (78), mkazi wa Mtaa wa Mtamba, Msasani jijini Dar es
Salaam, juzi Alhamisi alizimia baada ya kupata taarifa za mkewe, Saida
Abdalah ‘Mama Hamisi’ (21), kunaswa kwa tuhuma za ukahaba na kupandishwa
kizimbani kwenye Mahakama ya Jiji.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa
Mama Hamisi alinaswa kwenye msako wa machangudoa uliofanyika usiku wa
kuamkia juzi maeneo ya Buguruni.
Akiwa kizimbani, Mama Hamisi alisomewa shitaka la kujiuza na mwendesha
mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timoth Lyon.
Baada
ya kusomewa shitaka lake, Mama Hamisi na makahaba wengine 13, walikana
kufanya...
No comments:
Post a Comment