
Msanii wa zamani wa Kundi la Kaole Sanaa. Mr Bomba amefariki dunia
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu
na kansa ya uvimbe wa kwenye ini.
Msiba utakuwa Buguruni Malapa jijini
Dar es salaam nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi. Mwili utaagwa
siku ya Jumatatu nyumbani kwake Buguruni na kusafirishwa kijijini kwao
Mpwapwa Dodoma siku hiyo ya Jumatatu kwa mazish...
"HAKUNA MFANYABIASHARA MKUBWA NCHINI ALIYEFANIKIWA B
ASILIMIA 48.3 YA WANAUME TANZANIA WAMEBAMBIKIWA WATOTO NA WAKE ZAO

Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu
nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa
watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
Takwimu
hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha
kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati
asilimia 51.68 ndio wazazi halali.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa
Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria
Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Dar es Salaam.
Ingawa hakutaja idadi kamili ya
waliojitokeza kupima..
..

MWENYEKITI
wa kampuni za IPP, Reginald Mengi ametoboa siri kuwa hakuna
mfanyabiashara wa Tanzania aliyefanikiwa katika biashara kubwa kwa
kusaidiwa na serikali bila ya kutoa rushwa.
Mfanyabiashara huyo ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania
(MOAT), alisema yeye aligoma kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali
jambo lililosababisha kupoteza fursa nyingi ambazo zingemfanya awe na
maendeleo zaidi ya aliyonayo hivi sasa.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada
katika uzinduzi wa ripoti ya uchumi na maendeleo barani Afrika kwa mwaka
2013, uzinduzi uliofanyika katika...
No comments:
Post a Comment