VITUKO na matukio ya hatari kwenye mikutano ya CHADEMA vimeendelea kushika kasi.
Mh John Mnyika akihutubia wakazi wa Ubungo
Jana Mbunge
wa Ubungo, John Mnyika alinusurika kupigwa na bomu la machozi
lililorushwa na polisi waliokuwa wakizuia kufanyika mkutano ulioitishwa
na chama hicho.
Tukio hilo
lilitokea katika eneo la Mabibo kwenye viwanja vya Sahara ambapo bomu
hilo lilimpata mtu aliyekuwa karibu na Mnyika anayeitwa Thomas Jerome,
aliyejeruhiwa sehemu ya paja.
Baada ya
kurushwa kwa bomu hilo, polisi walitaka kumchukua majeruhi huyo ili
wamweke kwenye gari lao apelekwe hospitalini, lakini Mnyika aliwaelekeza
wafuasi wa CHADEMA kumchukua kwa madai kitendo kilichofanywa na askari
hao kililenga kuficha ushahidi wa jambo hilo.
Polisi
waliokuwemo eneo la tukio waliamua kukubaliana na matakwa ya wafuasi wa
CHADEMA waliomchukua Jerome na kumpeleka hospitali ambako hali yake
inadaiwa inaendelea vizuri.
Akielezea
hali ilivyokuwa akiwa katika mkutano mwingine uliofanyika Ubungo, Mnyika
alisema polisi walifika katika viwanja vya Sahara wakiwa na magari
matatu kwa lengo la kutawanya wafuasi wa CHADEMA wasifanye mkutano
wakidai haukuwa na baraka za jeshi hilo.
Mnyika
alisema polisi hao walisema sababu ya kuuzuia mkutano huo ni uwepo wa
ziara ya Makamu wa Rais katika Wilaya ya Kinondoni, hivyo walikuwa
wameelekeza nguvu zao katika ziara hiyo, kwamba hawakuwa na uwezo wa
kuulinda mkutano wa CHADEMA.
“Nikiwa
nimejiandaa kupanda jukwaani ndiyo polisi walikuja kusema tuache
tusifanye mkutano, nilisogea karibu na gari kumlalamikia ofisa wa polisi
kwani kitendo cha kuahirisha mkutano kwa barua waliyoileta saa sita
mchana siku ya mkutano wakati sisi tuliwapa taarifa siku nne zilizopita
ilikuwa sio haki.
“Nilimwambia
ofisa huyo wa polisi kuwa nilikuwa najadiliana kwa simu na viongozi
wakuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Inspekta
Jenerali wa Polisi Said Mwema kumlaumu kutumika vibaya kwa Jeshi la
Polisi.
“Nilipokuwa
bado najibizana naye bila fujo zozote, bomu lilirushwa kutoka ndani ya
gari ya polisi na kupita karibu na mimi likamjeruhi mtu aliyekuwa karibu
yangu, ki ukweli nimeshangazwa sana na matumizi mabaya ya silaha za
moto,” alisema.
Aliongeza
kuwa katika purukushani zilizotokea baada ya bomu kupigwa, alipoteza
nyaraka mbalimbali alizokuwa amebeba kama ushahidi kuwaonyesha wafuasi
wa chama hicho hasa jinsi serikali ya CCM na wabunge wake walivyopitisha
kodi ya huduma za simu, na kodi ya laini za simu.
Slaa anena
Aidha katika
mkutano huo ambao awali ulitangazwa kuwa ungehutubiwa na Katibu Mkuu wa
chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, haukuweza kuhutubiwa naye kwa kile
alichosema kuwa watu wake wa usalama walimwambia mapema hali si salama
kwenye mkutano huo.
“Nilipata
taarifa kutoka vyanzo vyangu kuwa polisi walikuwa na mpango wa kuleta
fujo, hivyo nikaona kwa kuwa wanatuwinda nisingeenda kuhutubia, pengine
bomu lililomkosa Mnyika lilikusudiwa kwangu au kwa mwingine,” alisema
Dk. Slaa alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu baada ya
kutoonekana mkutanoni.
Bonyeza Read More Kuendelea
CCM waihofia CHADEMA 2015
MWENYEKITI
wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM, Sophia Simba amesema
anahofia CHADEMA wanaweza kunyakua Jimbo la Babati Mjini au Vijijini.
Simba
alisema CHADEMA inaweza kufanya hivyo iwapo viongozi na wanachama wa CCM
watabweteka na kutowahamasisha watu wengi kujiunga na chama hicho
tawala.
Kiongozi
huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa
Manyara kabla ya kuanza ziara yake ya siku tatu wilayani Babati.
Simba
alisema viongozi na wanachama wa CHADEMA wanajituma katika kufanya kazi
zao kichama, hivyo ni vema CCM wakaacha mazoea ya kuhamasisha kila
chaguzi zinapokaribia.
“Mnawaona
wenzetu wa CHADEMA wanavyohangaika huko kwa wananchi kutafuta wapiga
kura kwa nguvu, na hii inaleta wasiwasi kwamba ikifika mwaka 2015
wanaweza hata kunyakua Jimbo hapa Babati, aidha Mjini au Vijijini,”
alisisitiza Mwenyekiti huyo.
Alisema ili kuifanya CCM iwe imara ni lazima viongozi wa jumuiya zote ikiwemo ya vijana kuhamasisha watu kujiunga.
Simba alisema uhamasishaji huo ikibidi uendane na wanachama hao kutotoa ada za uanachama ili kuwavutia wengi zaidi.
“Tafuteni
wanachama kwa nguvu zenu zote, ikibidi hata msiwalazimishe kulipa ada za
chama na kuwaita wanachama wafu kwani mkiwaita wafu wataenda kwa
wenzetu wa CHADEMA wanakochukuliwa bure,” alisema Simba.
Alisema
miongoni mwa sababu zilizokifanya chama hicho kishindwe kwenye chaguzi
ni kutowajibika ipasavyo katika uhamasishaji wa kutoa mwamko wa kisiasa
kwa wanachama wake.
Simba
alisema hali ni tofauti kwa wapinzani wao ambao kila kukicha wamekuwa
wakihahangaika kwa wananchi huku wakifanya mikutano mbalimbali ya
kuwarubuni kisiasa.
Alisisitiza
kuwa viongozi wasiwachukulie kimzaha mzaha wapinzani wao kwani wanafanya
mikakati na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Tuache
kufanya kazi kwa mazoea, tunapofikiria sisi ni chama tawala na kubweteka
tukisubiri wakati wa kampeni tutaumia, wenzetu mnawaona,” alisema.

BAVICHA mwenyeji mkutano wa IYD
BARAZA la
Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), linatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa
Bodi ya Umoja wa Vyama vya Demokrasia Duniani (IYDU), utakaofanyika
kuanzia Julai 25 hadi 30, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa BAVICHA,
Deogratias Munishi, alisema mkutano huo utafunguliwa na Katibu Mkuu wa
CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na utafungwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman
Mbowe.
Alisema IYDU
inayoundwa na mataifa 81, katika historia Tanzania inakuwa nchi ya
kwanza kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa nchi za Afrika zilizoko Kusini
mwa Jangwa la Sahara.
“Hii ni heshima ya pekee kwa BAVICHA, CHADEMA, Vijana wa Tanzania na taifa zima kwa ujumla,” alisema.
Alisema
baraza hilo litatumia mkutano huo kuwapatia washiriki fursa ya kujua
kama demokrasia na mfumo wa vyama vingi nchini, tasnia ya habari na
nafasi yake katika maendeleo ya demokrasia, uzoefu wa kujenga jamii za
kidemokrasia kupitia mabadiliko ya katiba.
Munishi
alisema masuala mengine watakayojadili ni uwezeshaji na hali ya kiuchumi
ya vijana wa Afrika kwa mtazamo wa sera za CHADEMA na fursa na
changamoto kwa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha,
alisema mkutano huo utakuwa ni fursa ya kuitangaza Tanzania katika sekta
ya utalii kwa kuwa wanaamini kama taifa bado hawajafanikiwa kujitangaza
vilivyo kupitia nyanja hiyo.
Alisema
watoa mada katika mkutano huo watakuwa Mabere Marando (mwanasiasa
mwandamizi na wakili wa kujitegemea), Jaji Thomas Mihayo (Jaji Mstaafu,
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania), Wakili
Francis Stolla (Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania), John Mnyika
(Makamu wa Rais mstaafu wa IYDU) na Jenerali Ulimwengu (Mwandishi
mwandamizi).
Alisema
ujumbe wa IYDU utapata fursa ya kuwa na mazungumzo na Kiongozi wa Kambi
ya Upinzani Bungeni, Jumuiya ya Ulaya nchini na Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu nchini (LHRC). Pia ujumbe huo utakutana na Spika wa Bunge
la Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
No comments:
Post a Comment