
Haya ni mashairi aliyoyaandika Nay wa mitego kwenda kwa mtoto
wa Rais a.k.a Riz One akimtaka amwambie baba yake kuwa mtwara
hawataki korosho, wanataka gesi na pia Lowassa asiache kugombea
urais maana yupo tayari kumpigia kampeni-2015
----------------
MASHAIRI YAKE:
Naongea na Riz one hey Riz
One, we si mtoto wa raisi Riz one. Mwambie dingi yako Masela hawamuelewi
wamakonde wa Mtwara hawataki tena Korosho, wanaitaka ges si mtawaua na
mkong'oto?! Nani lafiki...
POLISI WAFANIKIWA KUMKAMATA MVUTA BANGI ANALIYEMUUA MDOGO WAKE KWA KUMKATA MAPANGA HUKO SINGIDA

Jeshi la polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata Elibariki Alphoce
(21) mkazi wa kijiji cha Kizega wilaya ya Iramba, anayetuhumiwa kumuua
mdogo wake Mariam (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya
msingi Kizega.Elibariki
anatuhumiwa kumuua mdogo wake Mariam Julai 16 mwaka huu katika kijiji
cha Kizega kwa kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na
kisha kuteganisha kichwa na kiwiliwili.Ilielezwa kuwa Elibariki ni mtumiaji sugu wa madawa ya kulevya aina ya bangi.Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema
mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 18 mwaka huu akiwa amejificha kando
kando...
"WAGANGA MSITOE DAWA KWA MAJAMBAZI ILI TUSIWAKAMATE....TUPENI DAWA SISI ILI TUWAKAMATE"
Inaripotiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Polisi katika wilaya ya Mufindi, PCD
Ambwene Manyasi amewataka waganga wa jadi kuacha mara moja kuwapatia
majambazi dawa za kutokukamatwa na polisi, na badala yake waganga hao
wawapatie askari polisi dawa za kuwaona na kuwakamata wahalifu.Eliasa
Ally wa gazeti la Majira anaripoti kutoka Mufindi kuwa kauli na wito
huo umetolewa na OCD huyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mufindi,
wakati akizungumza na waganga wa jadi na tiba asilia kutoka Mudindi.OCD
amesema ni jukumu la kila mwananchi kuuchukia uhalifu na kulisaidia
jeshi la polisi kutimiza wajibu wake. Amenukuliwa akisema ifuatavyo:"Ninyi
waganga wa jadi na tiba asili kazi yenu kubwa ni kutibu magonjwa
yanayowasibu watu na siyo kutibu mbinu za majambazi ili wasiwe
wanakamatwa wanapofanya uhalifu,...
HUYU NDO MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

MSHTUKO mkubwa ulijiri Jumamosi iliyopita, ikiwa ni baada ya kusambaa
kwa habari za kumwagiwa tindikali, mfanyabiashara mwenye ‘levo’ ya
ubilionea, Said Said Mohammed, 42, ambaye ndiye mmiliki na Mkurugenzi
Mkuu wa Home Shopping Centre.
Said ambaye kwa utambulisho mwingine
anajulikana kama Said Mohammed Saad, alimwagiwa tindikali Ijumaa
iliyopita, saa 2 usiku, lakini habari zake zikavuma Jumamosi, hivyo
kuibua taharuki ya aina yake.
Kuhusu nani alimmwagia tindikali hiyo,
sababu ya kutendwa unyama huo, yupi mhusika mkuu wa ukatili wenyewe na
malengo ya uharamia, kwa jumla, hayo ni maswali yanayoendelea kuitesa
familia yake,...
WALIOWAUA WANAJESHI WA TANZANIA WATAJWA.....NI KUNDI LA "JANJAWEED" LINALOUNGWA MKONO NA SERIKALI YA SUDAN

WAKATI miili ya wanajeshi saba ikiwa imeagwa jana katika Viwanja vya
Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, imeelezwa kuwa kundi la
Janjaweed linaloungwa mkono na serikali ya Sudan ndilo lililowavamia na
kuwaua askari hao nchini humo na kuwajeruhi wengine 17 .
Wanajeshi
hao wa Tanzania ambao walikuwa ni sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la
Umoja wa Mataifa (Unamid), walifanyiwa unyama huo Julai 13, mwaka huu
katika eneo la kusini mwa Darfur, nchini Sudan.
Kiongozi wa moja ya
makundi ya wapiganaji la Sudan Liberation Movement (SLM), Minni Mannawi
ameibuka na kuwatuhumu wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na
serikali...
"WAKATI KIKWETE AKIONGOZA KUOMBA KONDOMU KWA OBAMA, MAGAZETI NAYO YALIISHIA KUANDIKA HABARI YA KUSHIKANA VIUNO".... GODBLESS LEMA

CHAMA cha
demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuanza kutoa mafunzo ya kujihami
kwa vijana wao maarufu kama Red brigedi kuanzia Agosti mosi, mwaka huu.
Akitangaza
tarehe hiyo jana wakati wa mkutano wa chama hicho uliofanyika Mbalizi wilaya ya
Mbeya Vijijini, kiongozi wa ulinzi wa chama hicho kanda ya Nyanda za juu kusini
Lucas Mwampiki, alisema kuwa ameamua kuweka wazi adhima hiyo ili serikali
isiendelee kusumbuka kuwa inao uwezo wa kuwazuia.
‘’Polisi
msisumbuke kutafuta kuwa tutaanza lini, ni hivi, tutaanza tarehe 1, mwezi wa
nane mwaka huu’’ alisema Mwampiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwakibete
Jijini Mbeya.
Mgeni...
No comments:
Post a Comment