EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, May 12, 2015

TLP YA MLEMA YAKINGIWA KIFUA


Moshi. Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema ametajwa kuwa ni mpinzani mstaarabu kwa sababu ya kuweka kando itikadi za kisiasa na kushirikiana na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza shughuli za maendeleo.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM, (UVCCM), Sadifa Juma alisema anampongeza Mrema kwa uamuzi wake ambao umeonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa katika kuwatumikia wananchi.
Sadifa aliyasema hayo juzi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro juzi.
Sadifa yuko katika ziara ya kikazi ya kuimarisha jumuiya hiyo pamoja na chama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu mkoani Kilimanjaro.
Hata hivyo, alisema licha ya Mrema kufanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi, kwa sasa kiongozi huyo anapaswa kupumzika.
Kuhusu nafasi ya vijana katika uongozi, Sadifa alisema licha ya jumuiya hiyo kupigania vijana kushiriki katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, hatakubali kuona jumuiya na chama kinatoa fursa hiyo kwa vijana wasio na uwezo na wanaoweza kukiletea matokeo mabaya chama hicho.
Awali, Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Kilimanjaro, Fred Mushi alisema jumuiya hiyo imeanza kutekeleza mipango inayolenga kukiimarisha chama chao ili kipate ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Katibu wa UVCCM mkoani hapa,  Yasin Lema aliwaonya vijana kuacha ushabiki wa kisiasa usio na manufaa kwao.
MWANANCHI,

No comments:

Post a Comment