EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, September 11, 2014

Dkt. Kebwe azindua rasmi Mfumo wa Uboreshaji wa Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja mkoa wa Dodoma.


 Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
Serikali imezindua rasmi Mfumo wa uboreshaji  na kusaidia  upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia Mzabuni mmoja Mkoa wa Dodoma.
mzuri na utakuwa shirikishi kwani utahakikisha kuwa jamii inapata mahitaji sahihi ya dawa na pia wanafanya wa sekta wanafanyakazi kwa bidii kwa lengo la kupambana na upungufu wa dawa unaoweza kujitokeza nchini.
Amesema kuwa moja ya vitu vikubwa wanavyovifanya sasa ni kutekeleza sera ya Matokeo Makubwa Sasa katika sekta ya afya kwani Barani Africa, Tanzania na Afrika ya Kusini zimekuwa nchi zinazojitahidi kufuata mifumo mizuri ya dawa kutokana na taarifa ya shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
“Mifumo hii itatusaidia na kuboresha mahitaji ya dawa katika vituo vya afya, na hivyo kupunguza vifo  mbalimbali  vinavyotokana na wananchi kutumia dawa na tiba ambazo sio sahihi kwa sababu ya kukosa dawa katika vituo vya afya”, alisema Mhe. Kebwe.
Hivyo Mhe. Dkt. Kebwe ameziagiza Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha zinatekeleza mfumo kwa ufanisi ili mikoa mingine ije kujifunza kutoka kwao kwa ajili ya kusaidia kupunguza upungufu wa dawa na vifaa vya tiba hapa nchini.
Amesema kuwa wananchi wanakwenda katika vituo vya afya wanapenda wakute huduma nzuri na za kuridhisha huku wakipata dawa na huduma nyingine za upimaji kwa gharama nafuu.
Aidha, Mhe. Dkt. Kebwe amefafnua kuwa, sasahivi wameamua kuja na mfumo huo kwa kuwa utasaidia sana kuboresha afya za wananchi na kutekeleza malengo ya Minelia.
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujipanga zaidi katika kufundisha na kuelekeza watumishi na kutengeneza mifumo mipya ambapo kwa ajili ya  kusogeza huduma karibu na wananchi kulingana na bajeti.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa msaada mkubwa  kwa Tanzania hasa mkoani Dodoma katika Wilaya husika kwani utasaidia kuboresha afya za wakazi wa Dodoma.
Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa anaamini kuwa mfumo huo utasimamia na kutekelezwa kama ilivyopangwa ili mikoa mingine ipate kuja kujifunza kupitia mkoa wa Dodoma.
“Naomba Mhe. Mgeni rasmi wakati tunasherehekea Uzinduzi huu, tuombe tupate mwongozo kwa udhibiti wa dawa zinazosambaa kwa kasi kupitia vyombo vya habari”, alisema Mhe. Nchimbi.
Mfumo huo utatoa fursa kwa Duka la Dawa la Bahari Limited kuzindua mfumo wa usambazaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya na Hospitali katika Wilaya zote saba za mkoa wa Dodoma.
Duka hilo limepewa jukumu hilo baada ya kushinda zabuni na hivyo linatarajiwa kupata fedha zake kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii, Mfuko wa Bima ya Afya na vyanzo mingine vya Halmashauri za Wilaya zote.
Mfumo huo ni wa kwanza kuanza kutekelezwa hapa nchini na kwa majaribio umeanzia mkoani Dodoma chini ya mradi tuimarishe Afya.

No comments:

Post a Comment