IRINGAHalmashauri ya Manispaa ya Iringa katika mwaka wa fedha 2013/14
ilipanga kutekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya
Tsh.4,723,360,853/=, kati ya fedha hizo Tsh.3,451,638,853 zilikuwa ni
ruzuku kutoka serikali kuu na wafadhili, na Tsh.1,271,722,000
zilitarajiwa kuchangiwa na Halmashauri kutokana na vyanzo vyake vya
ndani vya mapato.
: Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi (mwenye joho jekundu) ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Iringa akihutubia wajumbe wakati wa kikao cha baraza hilo jana. |
Michango ya wananchi na nguvu kazi katika kusaidia utekelezaji wa
miradi hiyo katika maeneo yao ilitarajiwa kufikia jumla ya Tsh.
266,398,000. Bajeti hiyo ilizingatia maelekezo, sera na miongozo kama
ilivyokuwa imetolewa na serikali.
Mhe. Mwenyekiti, Hadi kufikia Juni 2013/2014, Halmashauri ilikuwa
imepokea fedha za Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo jumla ya
Tsh.3,646,883,588 sawa na asilimia 77 ya makadirio, kati ya fedha hizo
Tsh.3,443,844,897 sawa na asilimia 95 ya fedha zilizopokelewa
zimetumika katika shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Iringa wakifuatilia kikao kwa umakini. |
No comments:
Post a Comment