KLABU ya Liverpool
inafanya majadiliano ya kutaka kumchukua Samuel Eto’o katika kipindi
hiki ambacho wanahitaji kusajili mshambuliaji. Eto’o kwasasa yuko huru
baada ya kuachwa na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita na anaweza
kuongeza uzoefu katika kikosi cha Liverpool kinachonolewa na Brandan
Rodgers. Rodgers amekuwa akitafuta mshambuliaji toka dili na Loic Remy
lilipokwama na Eto’o anaweza kuchagua lao sahihi. Uzoefu wa nyota huyo
mwenye umri wa miaka 33 hususani mataji matatu aliyoshinda ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya unaweza kumsaidia kwasababu Liverpool imerejea katika
michuano hiyo baada ya miaka mitano na hawana wachezaji wa kutosha wenye
uzoefu nayo. Mbali na Liverpool kuonyesha nia na Eto’o, Inter Milan na
Ajax Amsterdam nazo pia zimezungumza na wawakilishi wa mchezaji huyo.
CABALLERO ATAMBA KUCHUKUA NAMBA YA JOE HART, CITY.
GOLIKIPA mpya Willy
Caballero ana hamu kubwa ya kuchukua nafasi ya Joe Hart kama golikipa
namba moja wa Manchester City msimu huu. Kipa huyo wa kimataifa wa
Argentina alisajiliwa akitokea Malaga Julai ambapo alicheza katika mechi
yake ya kwanza ya kimashindano akiwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu wakati
walipotandikwa mabao 3-0 na Arsenal katika mchezo wa Ngao ya
Jamii. Caballero amesema anatamani kuendelea kubakia katika nafasi hiyo
wakati kikosi cha City kinachonolewa na Manuel Pellegrini kitakapoanza
kutetea taji lake katika mchezo dhidi ya Newcastle United Agosti 17
mwaka huu. Kipa huyo alikiri kuwa anataka kuwa namba moja wakati
akihojiwa na atafanya mazoezi kwa bidii ili kuhakikisha anamshawishi
kocha wake kumpa nafasi ya kuanza.
CHAMA CHA SOKA ITALIA CHAPATA RAIS MPYA.
CHAMA cha Soka nchini
Italia kimepata rais mpya Carlo Tavecchio aliyetangazwa jana. Tavecchio
mwenye umri wa miaka 71 alikuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo toka
mwaka 2009 lakini alithibitisha kugombea kugombea nafasi hiyo kufuatia
uamuzi wa Giancarlo Abete kuamua kujiuzulu baada ya Italia kutolewa
mapema katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil Juni mwaka
huu. Pamoja na kampeni zilizojaa utata huku akituhumiwa kwa masuala
mbalimbali Tavecchio alipambana na kuhakikisha anamshinda mpinzani wake
ambaye ni nyota wa zamani wa AC Milan Demetrio Albetini na kuteuliwa
kuwa rais mpya wa FIGC. Kibarua cha kwanza cha Tavecchio kitakuwa ni
kusaidia kutafutwa kwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo huku
kocha wa zamani wa Juventus Antonio Conte akipewa nafasi kubwa ya
kuchukua nafasi hiyo.
GFA YAUNDA KAMATI KUIIMARISHA BLACK STARS.
CHAMA cha Soka nchini
Ghana-GFA kimeunda kamati ya watu watatu itakayokuwa na jukumu la kuteua
mshauri wa ufundi katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, Black
Stars. Hata hivyo maofisa wa GFA wamesisitiza kuwa mshauri wa ufundi
atakayeteuliwa atakuwa na jukumu la kusimamia mfumo mzima wa Stars na
sio kocha pekee. Umuazi wa kuteua kamati hiyo kwa mujibu wa taarifa ya
GFA umepelekwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho
kufuatia kupitia muelekeo wa ufundi wa kikosi cha timu ya taifa. Kamati
hiyo ya watu watatu itaongozwa na makamu wa rais wa GFA Fred Crentsil
ambaye atafanya kazi sambamba na Fred Pappoe na Francis Oti
Akenteng. Taarifa ya GFA iliendelea kudai kuwa kamati hiyo itafanya
pamoja na kocha wa Black Stars Kwesi Appiah ili kutafuta mtu atakayeweza
kuipeleka timu ya taifa katika muelekeo unaofaa.
ANCELOTTI AWASHUSHUA WANAOMTAKA KHEDIRA, ADAI HANA MPANGO WA KUMUUZA.
MENEJA wa klabu ya Real
Madrid, Carlo Ancelotti amevionya vilabu vya Arsenal na Chelsea kumuacha
Sami Khedira kwani kiungo huyo hauzwi. Nyota huyo wa kimataifa wa
Ujerumani amekuwa akihusishwa kuondoka Santiago Bernabeu toka
waliposhinda Kombe la Dunia mwezi jana huku Uingereza pakitajwa kama
kama uelekeo wake. Usajili wa Mjerumani mwenzake Toni Kroos kutoka
Bayern Munich ndio ulionekana kuchangia kwa kiasi kikubwa nyota huyo
kuhusishwa na kuondoka lakini Ancelotti amekanusha tetesi hizo na kudai
kuwa Khedira bado ana mkataba nao unaomalizika kiangazi mwakani hivyo
bado atabakia klabu hapo kwa kipindi hiki. Madrid wanahatarisha kumkosa
Khedira bila kupata chochote kama wakishindwa kumshawishi asaini mkataba
mpya wa mabingwa hao wa Ulaya wakati wa msimu 2014-2015.
No comments:
Post a Comment