Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimshukuru Ofisa wa
Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa
(kushoto) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada
uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa
kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Wapili kushoto
ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kulia ni Mkuu wa Kikosi
cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano
hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani, kutoka kwa Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya
Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (watatu kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani inatarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,
Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa
Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha
zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment