EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, August 13, 2014

GARI YA WAANDISHI WA HABARI WA TEAM KWANZA JAMII YAPATA AJARI HUKO IRINGA

Mfanyakazi wa Kwanza Jamii Mathias Canal Mwenye T,Shirt Nyeus Akisaidiana na raia wema kuliondoa gari lililopata ajari kichakani.
Mathias Canal
Iringa.

 Moja kati ya wafanyakazi wa kituo hicho ambaye naye alikua miongoni nmwa abiria wa gari hiyo MATHIAS CANAL alieleza namna ajari hiyo ilivyotokea na kumshukuru mungu pamoja na wote waliowasaidia mara baada ya kutokea ajari hiyo.
mathias alieleza kama ifuatavyo..........
 
"Ajali hiyo imetokea maeneo ya Kijiji cha Ndolela, Tarafa ya Pawaga, Iringa vijijini wakati ikiwa imebaki kilomita moja kuweza kufika maeneo ambapo kulikuwa na mechi ya kumtafuta bingwa wa Tarafa, katika mashindano ya Spanest Cup 2014 yanayoendelea Tarafa ya Idodi na Pawaga.

 Gari hiyo ilikuwa na abiria wanne waandishi wawili, dereva pamoja na fundi mitambo.

"Ajali hiyo imetokea baada ya gari kuhamishwa njia na kokoto zilizopo barabarani hivyo kuingia porini ambapo hata hivyo tulitumia takribani masaa matatu kuitoa gari hiyo kwenye msitu kwa msaada wa vijana ambao tuliwatafuta huko kijijini."


"Abiria wote tumetoka salama isipokuwa majeraha madogomadogo ambayo tuliyapata.gari imeharibika hivyo kwa sasa ipo gereji kwa ajili ya service."

"Mungu ni mwema tunamshukuru kwa kututoa salama lakini pia tunawashukuru vijana wote waliotupatia msaada wa kuitoa gari msituni kwa kuibeba juu juu."
 TEAM SWACOTZ INAWAPA POLE WAFANYAKAZI WA TEAM KWANZA JAMII KWA DHARULA HIYO MUNGU AWALINDE KATIKA MAJUKUMU YAO.

No comments:

Post a Comment