EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, July 15, 2014

HII NDIO RATIBA KAMILI YA EURO 2014 ITAKAYOANZA KUTIMUA VUMBI SEPTEMBER 7 MWAKA HUU HUKO NCHINI UFARANSA

MABINGWA WA DUNIA wapya, Germany, watarudi dimbani tena kwenye Mashindano rasmi hapo Septemba 7 kuanza kampeni ya kutinga Fainali za EURO 2016 zitakazochezwa huko France Mwaka 2016.

Germany, ambao wako Kundi D la EURO 2016, wataanza kucheza Nyumbani na Scotland.
EURO2016-FRANCE_LOGOKabla ya Mechi hiyo, Germany watacheza Mechi ya Kirafiki huko Dusseldorf hapo Septemba 3 na Argentina, Timu ambayo ndio waliibwaga kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Maracana, Rio de Janeiro, Nchini Brazil kwa Bao 1-0, kwa Bao la Dakika ya 113 la Mario Götze.GERMANY-BINGWA2014
Mechi hii ya Kirafiki ilipangwa kabla hata ya kujulikana kama Nchi hizo zitakutana Fainali ya Kombe la Dunia.
Baada ya kuanza na Scotland, Mechi nyingine za Kundi D kwa Germany ni dhidi ya Poland, the Republic of Ireland, Gibraltar na Georgia.

Netherlands, ambao walimaliza Nafasi ya Tatu kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, wako Kundi A na wataanza na Czech Republic hapo Septemba 9 lakini safari hii watakuwa chini ya Kocha mpya, Guus Hiddink, anaerithi mikoba ya Louis van Gaal ambae amehamia kuwa Meneja mpya wa Manchester United.
England wao wako Kundi E na wataanza Ugenini na Switzerland hapo Septemba 8.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands.
KUNDI G: Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Mechi za Ufunguzi za EURO 2016 zitachezwa kwa Siku 3 mfululizo kuanzia Septemba 7 hadi Septemba 8.
Wenyeji France wao hawamo kwenye Makundi wanatarajiwa kucheza Mechi ya Kirafiki hapo Septemba 7 dhidi ya Serbia.
Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia Fainali.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 2014 hadi Oktoba 2015 na Ratiba kamili itatolewa na UEFA baada ya Droo.
Fainali za UEFA EURO 2016 zitachezwa Nchini Ufaransa kuanzia Juni 10, 2016 hadi Julai 10, 2016 na kwa mara ya kwanza Fainali hizo zitakuwa na Nchi 24 badala ya zile 16 za kawaida.
EURO 2016
RATIBA
Jumapili Septemba 7
19:00 Denmark v Armenia [Kundi I]
19:00 Hungary v Northern Ireland [Kundi F]
19:00 Georgia v Ireland [Kundi D]
21:45 Germany v Scotland [Kundi D]
21:45 Faroe Islands v Finland [Kundi F]
21:45 Greece v Romania [Kundi F]
21:45 Portugal v Albania [Kundi I[
21:45 Gibraltar v Poland [Kundi D]
Jumatatu Septemba 8
19:00 Russia v Liechtenstein [Kundi G]
21:45 Luxembourg v Belarus [Kundi C]
21:45 Austria v Sweden [Kundi G]
21:45 San Marino v Lithuania [Kundi E]
21:45 Spain v Macedonia [Kundi C]
21:45 Estonia v Slovenia [Kundi E]
21:45 Switzerland v England [Kundi E]
21:45 Ukraine v Slovakia [Kundi C]
21:45 Montenegro v Moldova [Kundi G]
Jumanne Septemba 9
19:00 Kazakhstan v Latvia [Kundi A]
19:00 Azerbaijan v Bulgaria [Kundi H]
21:45 Croatia v Norway [Kundi H]
21:45 Norway v Italy [KundiH]
21:45 Czech Republic v Netherlands [Kundi A]
21:45 Iceland v Turkey [Kundi A]
21:45 Andorra v Wales [Kundi B]
21:45 Bosnia/Herzegovina v Cyprus [Kundi B]
21:45 Israel v Belgium [Kundi B]

No comments:

Post a Comment