EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, July 14, 2014

HII NDIYO KAULI YA MOURINHO KUHUSU MESS

NAHODHA wa Argentina Lionel Messi amebebeshwa lawama na baadhi ya Watu baada ya Nchi yao kufungwa na Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia Bao 1-0 Jumapili Usiku hko Brazil lakini Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza Mchezaji huyo bado ni bora.

MESSI-WCFAINALI-HUZUNIMessi, Mchezaji wa Barcelona na ambae alitwaa Tuzo ya FIFA ya Mpira wa Dhahabu huko Brazil, ikimaanisha ndie Mchezaji Bora wa Fainali hizo za Kombe la Dunia, amekuwa akipondwa kwa kupewa Tuzo hiyo na hata Muargentina mwenzake, Lejendari Diego Maradona, amesema hakustahili.MOURINHO-CHELSEA_TRAINING

Lakini Mourinho amemtetea na kudai hahitaji kutwaa Kombe la Dunia ili atambulike ndie Mchezaji Bora kupita wote kwa wakati wote.
Mourinho amesema: “Ni rahisi kumheshimu akishinda lakini akipoteza si rahisi. Lakini bado yeye ni Mchezaji wa Kihistoria. Hahitaji kuwa Bingwa wa Dunia awe Mchezaji wa Kihistoria hasa kwa Muongo uliopita. Kwangu mimi Pele ni Pele na Maradona ni Maradona. Si juu yangu kufananisha Wachezaji wa Vizazi tofauti!”
Akizungumzia Argentina kufungwa na Germany na kulikosa Kombe la Dunia, na hasa Messi kulaumiwa kwa mchango wake hafifu, Mourinho amemtetea Messi na kudai alicheza vizuri mno Kipindi cha Kwanza lakini Argentina walifanya kosa kumtoa Lavezzi na kumwingiza Sergio Aguero kitu kilichomfanya Messi apoteze nguvu kwa kuzunguka sana Uwanjani.
Mourinho ameeleza: “Nataka kujua kwa nini walimtoa Lavezzi. Argentina walikuwa wakicheza na Misitari miwili ya Watu Wanne huku Enzo Perez akimkaba Phillipp Lahm pembeni na Lavezzi kufanya hivyo upande mwingine. Kwa sababu walikuwa imara, Messi aliweza kutembea tu wakati wakijihami na akipata Mpira alikuwa na na nguvu ya kukimbia na kuleta tofauti.”
Aliongeza: “Baada Sabella kumwingiza Aguero na kumtoa Lavezzi, Argentina walibadili Mfumo kutoka 4-4-2 kwenda 4-3-3 na kupoteza uwiano. Sasa ikabidi Messi akimbie sana baada Lavezzi kutoka. Timu ikapoteza uwiano na nguvu yao, kitu ambacho walikihitaji sana Dakika za Nyongeza 30!”

No comments:

Post a Comment