EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, May 3, 2014

Mtemvu,Azzan na Zungu wawandalia mashindano ya mpira vilabu vya jogging Dar, Ngoma itaanza kupigwa Mei 10 Karume




NA MSHAMU NGOJWIKE
MICHUANO ya  soka kwa timu maalum za mazoezi ya viungo zinazojulikana kama ‘Jogging’  inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 10 mwaka huu katika Uwanja  wa Karume, jijini Dar  es Salaam.
timu za mbio za pole'jogging'wakikimbia barabarani
        wakimbia jogging wakiwa mazoezini hapo kazi ipo mei 10     ufunguzi karume
 wanaume kazini hapo wakikatisha katika kati ya mji na mazezi yao

Mashindano hayo yanayoandaliwa na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kwa kushirikiana na wabunge wa Ilala, Kinondoni na Temeke yatahusisha jumla ya timu 95 kutoka mkoani humu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Mashindano hayo, Marijani  Rajab, alisema  lengo la  mashindano hayo ni kuwakutanisha wanamichezo wa jijini Dar es Salaam ili kutafuta namna ya kuendeleza mchezo huo.



baadhi ya timu zikifanya mazoezi ya kukimbia

Alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia pikipiki ya miguu mitatu, wakati yule pili ataondoka na bodaboda bila kusahau mshindi wa tatu atakayepewa zawadi itakayojulikana baadaye.
Kwa upande mwingine Katibu  wa DRFA, Msanifu Kondo alisema kwa baada ya kushirikisha timu za wanaume, maashindano ya mwakani pia yatashirikisha wanawake.
“Kutokana na ugeni wa mashindano haya tumeona bora tuanze na timu za wanaume, ila tunaamini mwakani wanawake pia watashiriki kwa namna moja ama nyingine,
mara baada ya kumaliza tutaanza mikakati ya kuhamasisha  wanawake ili nao waweze kushiriki na kuongeza hamasa ndani na nje ya mkoa,”alisema

wakati huo huo, ametowa wito kwa vilabu vingine kujitokeza na kuthibisha kushriki kwani hadi hivi sasa ni Camp za Jogging 45 ndizo zilizothibisha kushiriki,na mwisho wa kuthibisha ni Hiyo mei 10 siku ya ufunguzi.


No comments:

Post a Comment