Katibu
mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye akizungumza katika moja ya semina ya
FIFA iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni.
BARAZA la vyama vya soka ukanda
wa Afrika mashariki na kati, CECAFA limeungana na nchi ya Somalia
kuomboleza kifo cha mtoto mmoja mcheza mpira na wengine wawili
kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililotegwa katika uwanja wa wazi
mjini Balanbale karibu na mpaka wa Ethiopia.
Mwa mujibu wa taarifa iliyotumwa
katika mtandao huu na Afisa habari wa chama cha soka nchini Somalia,
Shafi’i Mohyaddin Abokar imesema ili kuungana na Somalia katika kipindi
hiki kigumu baada ya tukio hilo la kuhuzunisha, katibu mkuu wa CECAFA
Nicholas Musonye ametuma salamu za rambirambi kwa katibu mkuu wa chama
cha soka nchini Somalia Abdi Qani Said na kutoa pole kwa taifa hilo
changa katika maendeleo ya soka.
“Nimesoma habari za kuhuzunisha
juu ya kifo cha mchezaji kijana na wawili kujeruhiwa wakati wakicheza
mpira nchini Somalia. Naungana na wewe na familia ya mtoto aliyefariki
katika kipindi hiki cha huzuni”. Alisema katibu wa CECAFA katika barua
yake ya salamu za rambirambi kwa katibu mkuu wa chama cha Somalia jana
jioni.
Bwana Musonye alisema CECAFA siku
zote inaamini kuwa ipo siku itatokea Somalia yenye utulivu ambapo
maendeleo ya mpira yatapatikana na wachezaji wake watajitangaza
kimataifa.
“Tunaamini wachezaji wawili
waliojeruhiwa wataendelea vizuri na tunawaomba wazazi wawe wavumilivu
wakati huu wa huzuni” . Musonye aliendelea katika barua yake ya Salamu
za rambirambi.
No comments:
Post a Comment