EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, April 22, 2014

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA KANISA KUPITIA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna TibaijukaWAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, amesitisha ujenzi wa Kanisa la ‘Hemba Ministries’ linalojengwa katika Kitongoji cha Busimba, Kijiji cha Ihangiro, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera.
Hatua hiyo ya Prof. Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini inatokana na ujenzi wa kanisa hilo kufanyika bila kufuata utaratibu wa wamiliki kupata vibali vya ujenzi vya kuhakikisha liko salama.
Wakazi wa kitongoji hicho wamekuwa katika mgogoro mkubwa na mchungaji wa kanisa hilo kwa muda mrefu sasa, wakimtuhumu kuanzisha kanisa katika makazi yao bila kufuata utaratibu na kuhubiri uchochezi kwa waumini wa madhehebu mengine.
Kabla ya Waziri Tibaijuka kutembelea eneo hilo wiki iliyopita, viongozi wa kitongoji hicho, kijiji pamoja na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Muleba (OCD) kwa agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Limbris Kipuyo, waliwahi kufika na kuagiza ujenzi huo usitishwe hadi utaratibu wa vibali utakapofuatwa.
Hata hivyo, mchungaji wa kanisa hilo amekuwa jeuri kwa kutotii maagizo hayo badala yake ameendelea na utatatibu wake wa kuendesha maombi usiku kucha, hali ambayo imekuwa inaleta usumbufu mkubwa kijijini hapo.
Katika mawasiliano na gazeti hili, Waziri Tibaijuka alisema kuwa ametembelea eneo husika na kusitisha ujenzi wa kanisa hilo ambalo linahitaji vibali vya ujenzi kuhakikisha liko salama.
“Nimesikia wamekaidi agizo langu, kwa hiyo natoa nakala hii pia kwa mkuu wa wilaya ili aagize mhandisi kwenda kujionea nini kinaendelea ili kunusuru maisha ya watu. Jengo lilionekana kama halina uimara wowote,” alisema.

Desemba mwaka jana, Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Muleba, alitembelea eneo hilo akiwa na OCD na hivyo kutoa masharti kadhaa ya kumzuia mchungaji kufanya maombi usiku badala yake aishie saa 12 jioni.
Pia katika masharti hayo, wenye kanisa walitakiwa kupata kibali cha ofisa Utamaduni ili kuelekezwa aina ya vifaa vya muziki na vipaza sauti vya kutumia bila kuwasumbua wananchi wengine wanaozunguka eneo hilo.
Ofisa huyo pia alimwagiza mchungaji kuomba kibali kwa ofisa Afya ili kujenga vyoo vya kisasa vitakavyoweza kuhudunia waumini badala ya kuharibu mazingira kwa kujisaidia shambani na vichakani.
SOURCE>>>TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment