EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 6, 2014

TAARIFA ZA GHAFLA KWA YANGA MECHI YAO NA AL AHLY YAPEWA UHAMISHO

ALEX STADIUM
Baada ya ukimya na utata, sasa imetangazwa kuwa mechi kati ya mabingwa Afrika, Al Ahly na wale wa Tanzania Bara, Yanga itapigwa kwenye Uwanja wa Max mjini Alexandria.

Mji huo uko kwenye pwani ya bahari ya Mediterranean, kilomita zaidi ya 200 kutoka katika jiji hili la Cairo, mwendo wa zaidi ya masaa mawili.

Awali ilikuwa siri, lakini leo mchana  kiongozi wa umoja wa klabu za Misri, Tharwat Swelam ameviambia vyombo vya habari mechi hiyo itapigwa bila ya mashabiki.

“Lakini muda utakuwa ni saa moja usiku (saa mbili Bongo) kama ilivyopangwa awali, pia hatutaruhusu mashabiki,” alisema.
Kutokana na uamuzi huo, Yanga sasa inalazimika kusafiri tena kwenda Alexandria nab ado uongozi wake haujatoa msimamo wake.
Awali uongozi wa Yanga ulisema kama mechi itachezwa Alexandria basi lazima wapewe ndege, lakini mchana huu uongozi wa Al Ahly umeliambia Championi Ijumaa kuwa bado uko katika sheria za Caf..

“Mechi ikibadilishwa baada ya siku tatu kabla ya siku iliyopangwa hakuna tatizo kwa sheria za Caf na pake Alexandiria si mbali,” alisema Mohamed Mowad ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya habari.
Suala hilo lilikuwa na utata mkubwa, lakini mwisho limefikia hapo na ainaonekana Al Ahly wana hofu ya kufanyiwa fujo na mashabiki wao iwapo watapoteza mchezo huo.


Lakini Watanzania wanaoishi hapa wanasema hizo ni mbinu za kuwavuruga Yanga ili wazidi kuchanganyikiwa.
Baadaye jioni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema amepata taarifa hizo na tayari analifanyia kazi.

"Kweli tumepata taarifa hizo na tayari tumeanza kulifanyia kazi suala hilo," alisema Sanga.
SOURCE: CHAMPIONI

No comments:

Post a Comment