NA: KASSIM NGUMBI
WANAFUNZI watano wanaosoma vidato tofauti katika shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo, wamefariki dunia mapema jana, kufuatia kukanyangwa na gari ndogo aina ya Mercedez Benz, wakati wakiwa katika mchakamchaka wa asubuhi katika barabara kuu ya Mtwara kwenda Dar es salaam, maeneo ya Msijute.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephine, akiwa ndandi ya
wodi namba moja katika Hospitali ya mkoa ya Ligula, alipokwenda kuwaona
majeruhi wa ajali ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mustafa
Sabodo, iliyotokea leo katika barabara ya Mtwara Lindi wakati wanafunzi
wa shule hiyo wakikimbia mchakamchaka asubuhi. Kushoto Kaimu Katibu
tawala wa Mkoa Smythies Pangisa. Katika ajali hiyo iliyohusisha gari
ndogo aina ya Masdz Benzi lenye namba za usajili T174 AEB imesababisha
vifo vya wanafunzi wanne na wengine 47 kujeruhiwa
Kwa mujibu wa taarifa ilizozifikia chumba cha habari cha Pride Fm Radio, kutoka kwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara ACP Zelothe Stephen zimetaja wanafunzi waliofariki katika tukio hilo kuwa ni pamoja na Hilda Mathias Nguli, Khailat Mohammed Saidi, Mwanahamisi Hassan Mohammed, Nasma Salum Mkunja na Farida Ally.
Amesema kuwa mwanafunzi mmoja alifariki papo hapo eneo la tukio baada ya kukanyagwa kabisa na gari hilo, wawili walifariki njiani na mmoja alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya ligula kwa matibabu zaidi.
Mmoja wa majeruhi akipelekwa wodini baada ya kupokewa katika hospitali hiyoKamanda Zelothe amesema kuwa jumla ya wanafunzi 51 walikutwa na mkasa huo, ambapo kati ya hao wanafunzi 46 wamejeruhiwa, huku wanafunzi 28 wakitibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao, ambapo wanafunzi wengine bado wamelazwa wakiendelea na matibabu.
Kamanda wa Polisi, Zelothe Steven akizungumzia ajali hiyo
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya Ligula Mohammed Gwao amesema kuwa wanafunzi wawili Joel Simon miaka (13) na Sabaha Badilu miaka (13), wamehamishiwa katika hospitali ya Nyangao kwa matibabu zaidi ya mifupa, na hivyo kubaki na majeruhi 17 wanaondelea kupokea matibabu katika hospitali hiyo ya Ligula.
Kamanda Zelote akikagua gari lililohusika katika ajali hiyo
Kamanda huyo amesema kuwa dereva wa gari hilo
aina ya Mercedez Benzi Station Wagon, lenye namba za usajili T 174 AED Mbaraka
Bakari Mgwegwe mfanyabiashara mwenye umri wa miaka (50) anashikiliwa na jeshi
la polisi kwa mahojiano na uchunguzi kamili wa ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment