EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, November 25, 2013

AFRIKA MASHARIKI YAOMBWA KUFUNGUA MIPAKA KUTETEA WALIYOKUBALIANA


Jackline Mugo-M/kiti EAEO

Chama cha Waajiri cha Afrika Mashariki (E.A.E.O), kimewaomba viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (E.A.C), kufungua mipaka na kutekeleza masuala waliyokubaliana, ili nchi zao zisafirishe bidhaa, kuwa na ajira, huduma na mitaji bila vikwazo vyovyote.
Jacqueline Mugo Mwenyekiti wa chama hicho, pamoja na Makamu wake, Francis Atwoli, wamesema bado kuna vikwazo vingi katika utekelezaji wa makubaliano ya wakuu wa nchi hizo, na kueleza mtangamano kwa nchi za EAC ni kitu cha maana ili kuleta maendeleo.


 Mugo amesema, hadi sasa uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kufanya kazi kwenye nchi yoyote mwanachama, bado limekuwa suala gumu kwa kuwa bado halijapewa nafasi kubwa ya kupatiwa ufumbuzi kwa viongozi wa nchi husika na hata kwa vyama vya kijamii.
Kwa upande wake Atwoli amesema kuwa ni aibu kuona wataalamu wa fani mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ndani ya nchi wanachama na kwenda kufanya nchi za Ulaya au Marekani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk.Aggrey Mlimuka, amesema kuwa kila nchi ina mambo yake, ambayo bado hawajayafungua hivyo hakuna sababu ya kutupiana lawama.

No comments:

Post a Comment