EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 9, 2013

WAWEKEZAJI BOMU NCHINI KUNYANG'ANYWA MAENEO YAO



NA: FARAJI MAARUFU
Serikali imeagiza viongozi na watendaji wa Halmashauri nchini, kuwanyang’anya maeneo baadhi ya wawekezaji, ambao hununua maeneo makubwa kwa lengo la kuombea mikopo badala ya kuyaendeleza.
Kauli hiyo imetolewa na rais Jakaya Kikwete mjini Kibaha mkoani Pwani, wakati akipokea taarifa ya halmashauri hiyo, na kuwataka viongozi wa halmashauri husika zitakazobaini wawekezaji  wa aina hiyo, kuwabana watumie ardhi vizuri wanayopewa kwa maslahi ya eneo husika.
Amesema kuwa rasilimali ya kuongeza maendeleo ni ardhi, hivyo kama itatumika vibaya itasababisha kudidimiza maendeleo kwa kiasi kikubwa.
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIHUTUBIA WANANCHI
Rais Kikwete aidha amesema kuwa baadhi ya wawekezaji wamejenga tabia ya kuweka dhamana maeneo wanayopatiwa, kwa lengo la kuyauza kwa gharama kubwa baadaye, au kuyachukulia mikopo na kwenda kuendeleza mikoa jirani hususani jijini Dar es Salaam.
                                            
                                      

No comments:

Post a Comment