Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iko kwenye mchakato wa kubadilisha mfumo wa upangaji za mitihani ya sekondari na matumizi ya alama za maendeleo ya mwanafunzi.
![]() |
WAZIRI WA ELIMU tz |
Mfumo huo ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwenye Mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka huu, unakuja ikiwa ni miezi michache tangu Tume ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kufeli kwa maelfu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012.
Akizungumzia mchakato huo, Kamishna wa Elimu Profesa Eustella
Bhalalusesa amesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu na kuwa haina uhusiano na taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu ambayo mpaka sasa haijawekwa hadharani. Amesema kuwa, ili kuweza kuboresha vyema mfumo huo wameshirikisha wadau mbalimbali zikiwamo shule za sekondari.
Bhalalusesa amesema kuwa, hadi sasa wameshapokea zaidi ya asilimia 60 ya maoni hayo kutokana na lengo walilojiwekea, katika kukusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na cha sita pamoja na matumizi ya ‘Alama Endelevu ya Mwanafunzi.
No comments:
Post a Comment