EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, October 17, 2013

KAMATI YA UCHUMI YA UN YAKUTANA ADDS ABABA KUIJADILI AFRIKA



Umoja wa Mataifa umepanga kufanyika kikao chenye shabaha ya kujadili maendeleo ya nchi za Kiafrika, huko Addis Ababa mji mkuu wa nchi ya Ethiopia. 


Kamati ya Uchumi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, kikao hicho kitaanza kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uchumi wa Afrika imeeleza kuwa, kikao hicho kitaendelea hadi Novemba 5, na kuzishirikisha Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, washiriki wa kikao hicho watafanya juhudi za kufikia kwenye natija kuhusiana na mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele ambayo yatakuwa chachu ya maendeleo imara barani Afrika.
Kamati hiyo imeeleza kuwa, kikao hicho kitafanya juhudi pia za kupata uungaji mkono na misaada ya nchi wafadhili zenye lengo la kuboresha ustawi wa Afrika.

No comments:

Post a Comment