EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 16, 2013

NACTE YAVIKOROMEA VYUO VYA UFUNDI NCHINI



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi hapa nchini (NACTE), limeendelea kutoa tahadhari kwa jamii, na kuwataka wamiliki wa vyuo binafsi kukamilisha taratibu za kisheria, kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk.Primunus Nkwera, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambaye amesema kuwa uendeshaji holela wa sekta hiyo, ni sawa na kufanya makosa jinai katika mazingira ya wazi ambayo mamlaka hiyo haiwezi kufumbia macho.


Dk.Nkwera amesema kuwa wamiliki wote wa vyuo binafsi lazima watambue haki na wajibu wa kukamilisha kazi ya usajili wa vyuo hivyo kabla ya kuanza kwa majukumu yao ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa fedha kutoka kwa jamii.

Ameongeza kuwa kabla ya kukamilika kwa taarifa ya watafiti na wachunguzi wa masuala ya elimu, ambayo Nacte inatarajia kuipata hivi karibuni baada ya kukamilika, imeona vyema kutoa tahadhari kwa wale ambao bado hawajakamilisha taratibu zinazotakiwa.

Aidha, Dk.Nkwera, amewataka wazazi wanaowapeleka vijana wao katika vyuo hivyo, kuhoji mambo kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na usajili.

No comments:

Post a Comment