EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 16, 2013

BODABODA KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASILIAMALI



Madereva pikipiki maarufu kama Bodaboda wametakiwa kuanzisha vikundi, ili waweze kujikwamua na umaskini kutokana na ukosefu wa ajira kwa vijana uliopo hapa nchini.

Hayo yamezungumzwa na kiongozi wa kikundi cha bodaboda kilichopo maeneo ya kwa jionee mtaa wa Ligula C, kata ya Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani Hamza Hashimu Mjambe, ambaye amesema kwa kufanya hivyo kutaweza kuwajengea fursa ambazo zipo mkoani Mtwara na zitakazokuwepo hapo baadae.



Aidha Mjambe maarufu kwa jina la Mmuku amesema kuwa ni nyema kwa watu na makampuni binafsi kuweza kujitokeza kwa wingi kuyafadhili makundi hayo ya Bodaboda ili yaweze kujikwamua na umaskini uliopo hapa nchini.
Hivyo Mmuku pia amewasihii madereva pikipiki kutoa usafirishaji ulio bora zaidi kwa jamii husika, ili kuweza kujijengea uaminifu na usafishaji bora wa abiria kwa jamii husika.

No comments:

Post a Comment