EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, October 16, 2013

NAIBU RAISI WA KENYA ASEMA ATAENDELEA KUHUDHURIA VIKAO VYA KESI YAKE THE HEGUE NCHINI UHORANZI


Naibu Raisi wa Kenya-William Ruto

Naibu Rais wa Kenya William Ruto amewaambia waandishi wa habari mjini The Hague nchini Uholanzi anakohudhuria vikao vya kesi dhidi yake kuwa, ataendelea kuhudhuria vikao hivyo huku Kenya ikisubiri maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutoa maamuzi juu ya kuahirishwa kwa kesi dhidi yake na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Ruto alitumia maneno makali dhidi ya waendesha  mashtaka wa mahakama ya ICC akisema imebainika wazi kuwa utendaji kazi wao ulikuwa hovyo, na kwamba waliwashawishi mashahidi kwa kuwapa hongo ili kutoa ushahidi wa uwongo dhidi yake na washtakiwa wenzake.
 
Amesema pia kuwa yeye na Rais Kenyatta wanaitaka mahakama hiyo kuheshimu sheria za Kenya, na kuwaruhusu kuhudumia taifa lao kama viongozi waliochaguliwa kihalali na wananchi, na hivyo kuzisikiliza kesi hizo kwa muda uliotengwa na sio mfululizo, ili kuwe na mizani  ya kikazi upande wao kama viongozi na upande wa waendesha mashtaka.
  Mwishoni mwa wiki viongozi wa Umoja wa Afrika katika mkutano maalum mjini Addis Ababa, Ethiopia walitoa mwito kwa Baraza la Usalama kufikia azimio  litakaloahirisha kwa mwaka mmoja  kesi dhidi ya viongozi hao wa Kenya.Viongozi hao wa Afrika walimshauri Rais Kenyatta kutohudhuria vikao vya kesi dhidi yake vinavyotarajiwa kuanza Novemba 12 huko The Hague katika mahakama ya kimataifa –ICC.

No comments:

Post a Comment