EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 18, 2013

MIILI YA WATU NA BUNDUKI AINA YA AK 47 VYAGUNDULIKA WESTGATE



Wachunguzi wa Kenya wanaoendelea na uchunguzi katika jengo la Westgate lililokumbwa na tukio la kigaidi, wamegundua sehemu za miili ya watu na bunduki tatu aina ya AK 47. 
Jengi la kibiashara la WEstgate Kenya Baada ya kushambuliwa na Al shabab

Ofisa mmoja anayeshiriki kwenye uchunguzi huo amesema kuwa wamepata fuvu la mmoja wa watu wanaoamini kuwa ni magaidi wane, waliouawa kwenye operesheni ya uokoaji, huku Ofisa huyo akisema kuwa bado kuna miili na sehemu za miili ya watu kwenye kifusi cha jengo hilo.
Mwanzoni mwa mwezi huu wachunguzi waligundua gari iliyotumiwa na magaidi kwenda kufanya shambulizi, na hivi karibuni wamegundua vitu vingi vinavyosaidia katika uchunguzi.
Hadi sasa watu 40 wamekamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment